Burudani

Trump kuendelea kuwa mtayarishaji mkuu wa series ya Celebrity Apprentice

Inaonekana Donald Trump, hawezi kuyaacha maisha ya TV. Imeripotiwa kuwa Rais huyo mteule wa Marekani, ataendelea kuwa mtayarishaji mkuu wa reality series ya NBC, Celebrity Apprentice.

celebrity-apprentice

Kwa mujibu wa tovuti ya Variety, Trump ataendelea kutambulika kama executive producer wa show hiyo ambayo sasa itakuwa ikiongozwa na Arnold Schwarzenegger — itakaporejea tena, January 2 baada ya kutofanyika kwa miaka miwili.

Tovuti hiyo imedai kuwa, jina la tajiri huyo mwenye miaka 70, litatokea baada ya mwanzilishi wa show hiyo, Mark Burnett na kabla ya Schwarzenegger ambaye pia ni mtayarishaji mkuu.

Kutokana na kuendelea kuwepo kwenye credits licha ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani, Trump ataendelea kuingiza fedha kutokana na series hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents