Diamond Platnumz

Triple Threat: Tupogo, Number 1 na Roho Yangu

Tupogo namba moja na roho yangu, ni sentesi ya Kiswahili inayoweza kuleta maana sio? Ni sentesi yenye majina ya nyimbo tatu zinazokimbiza sasa hivi kwenye redio za Tanzania. Tupogo ya Ommy Dimpoz, Number One ya Diamond Platnumz na Roho Yangu ya Rich Mavoko.

page

Tutake tusitake, hawa watatu wameishikilia crown ya muziki pendwa wa Tanzania ambao umetoka kuwa Bongo Flava peke yake na kuwa muziki uliokopa ladha zingine za muziki wa Kiafrika hasa ule wa Nigeria. Hizi ndizo nyimbo zenye nguvu kiasi cha kuongeza misamiati mipya kwenye lugha ya Kiswahili. Mathalan, Tupogo na Ngololo kutoka kwenye wimbo wa Nasib Abdul. Kwa Kiingereza jina linalofaa kuzijumuisha pamoja, tunaweza kuziita, Triple Threat.

43603d04fa7d11e28d6322000ae811f0_7

Ilianza kutoka Tupogo ambayo baadhi ya watu walihisi kama Ommy kaingia choo cha kike hivi. Kwao Tupogo waliuona ni ‘Miss na sio Hit’. Kwa kuona mbali, nakumbuka niliandika makala maalum kuisifia na nikasema itampeleka mbali sana.

Ni kweli, licha ya kuwa anthem kwenye redio, Tupogo imegeuka kuwa hit kwenye sherehe hasa za harusi. Na kama wimbo wako ukiweza kuwa maarufu kwenye harusi ambako huhudhuriwa na watu wazima zaidi, hilo ni jibu tosha kuwa wimbo wako umefanikiwa, nenda kamata kinywaji ukipendacho, vuta stuli ndefu, jipongeze.

1186327_617322744956210_1893964897_n

Kwa upande wa Number 1, uzinduzi wa video yake tu ulionesha kuwa hit nyingine ya Bongo Flava Prince imewadia.

Ikiwa na video kali na ya gharama, Number 1 ilipigia mstari mnene wa jinsi Diamond alivyofika mbali. Kama ilivyokuwa Nataka Kulewa, scandal zikazuka. Dayna Nyange akaibuka na kudai beat yake imetumiwa na Diamond kufanya wimbo huo huku Baba Levo akiwa na lake pia, eti Diamond kamwibia chorus.

Watu tukahisi hilo linaweza kuwa jabari kubwa kama la Tsunami linaloweza kuangamiza career ya Diamond. Aaah wapi!! Kumbe walikuwa wanatafuta kick tu, wakatupwa kule na Number One ikaendelea kutongoza masikio ya mashibiki wa muziki na wakaipa ‘green light’.

Vodacom wakachukua fursa, wakamdaka na kumpa mkataba exclusive wa kuuza wimbo huo kama muito kwa wateja wao. nI Msanii gani mwingine amewahi kupata mkataba kama huo? Sikumbuki. Mungu, Vodacom na yeye mwenyewe ndio wanajua wamempa milioni mia ngapi, lakini nina uhakika si pesa ya madafu. Then what? Mafanikio yanabubujika tu kuelekea upande wake.

533253_617205484985892_433409233_n

Trilogy ikaja kumaliziwa na Rich Mavoko. Wimbo wa mapenzi ambao kwangu umeandikwa kwa ubora ninaoshindwa kuuelezea. Ni wimbo mtamu ambao nakuja kuupenda zaidi kwenye chorus na jinsi ambavyo anasikika kwa harmony ya juu inayozipa support sauti za chorus zilizosambaa vizuri kwenye mzunguko wa spika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents