Habari

Trey Songz akanusha kumdate Kelly Rowland

By  | 

Bingwa wa ‘baby making music” Trey Songz amezikanusha fununu kuwa anamdate Kelly Rowland, japo amekubali kuwa anatamani wangekuwa pamoja.

Mwanamuziki huyo wa R&B hivi karibuni ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Heart Attack,’ ambayo Kelly yumo na hivyo kuziongezea nguvu fununu za kuwa wanamuziki hao ni wapenzi.

Hata hivyo Trey hakuacha kumsifia mwanamuziki huyo wa ‘Motivation’: “anapoingia chumbani, hukifanya chumba chote king’ae, ni mkarimu na wakati wote huwa yuko vile vile kila unapokutana naye.”

Hivi karibuni imedaiwa kuwa Trey Songz ameachana na aliyekuwa mpenzi wake Lauren London baada Trey kukataa kuzaa naye mtoto.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments