Burudani

Touch Me ya AY yapata ‘green light’ kuchezwa Jamaica, Marekani soon

AY amesema wimbo wake Touch Me aliomshirikisha Sean Kingston unaendelea kufanya vizuri Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla na hivi karibuni utaanza kuchezwa Jamaica.

AY

AY ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo amepata rotation inayostahili na anaamini utaendelea kufanya vizuri zaidi.

“Wimbo unapata rotation kubwa sana. Umeingia kwenye chart kubwa mbalimbali,” amesema AY. “Unajua watu wangesema huu wimbo kafanya na mmarekani labda nini, lakini imekuwa tofauti sana sasa hivi unazidi kuchanganya zaidi. Sehemu kama Marekani bado lakini nimepata detailS za wiki ya pili itaanza kupigwa. Kulikuwa kuna process za Jamaica, nimeona wanaanza kupiga February na imeshapitishwa kwenye bodi ya muziki wa Jamaica,” ameongeza.

“Lakini hapa nyumbani, Kenya, Burundi, Nigeria na sehemu zingine za Afrika mambo yanaenda vizuri sana.”

P
K

Katika hatua nyingine AY amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kusubiri ujio wa wimbo wake mpya, Zigo.

“Ni wimbo ambao wasanii wengi wakiusikiliza wanatamani kuufanyia hata remix kutokana na wimbo jinsi ulivyo. Wengi wanatamani kuweka nguvu zao pia lakini nikaona ngoja nifanye mwenyewe hii kazi. Kwahiyo wimbo unatoka tarehe mbili mwezi wa pili. Lakini bado naumiza kichwa kwenye video sijui nifanye na nani? Kutokana NA wimbo wenyeye ulivyokaa sitaki kuuharibu. Watu wasubirie vitu vizuri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents