Habari

TLP: Mtengeni Maalim Seif hadi atakapoitambua serikali

Chama cha Tanzania Labour(TLP) kimemuandikia barua Rais wa Mapinduzi wa Zanzibar, Dk Mohamed Ali Shein na kumtaka kuanzia sasa wamtenge Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kutomualika kwenye shughuli zozote za kitaifa.

maalim-seif

Maalim Seif

Katika barua ya chama hicho iliyosainiwa na Mwenyekiti wake, Augustine Mrema ilisema chama hicho kimesikitishwa na wanalaani kitendo kilichofanywa na Maalim Seif wakati wa maziko ya marehemu Mzee Aboud Jumbe cha kukataa kumpa Rais Shein mkono wa kusalimiana.

Alisema kuleta tofauti za kisiasa msibani kwa makusudi, Maalim Seif ameendelea kuwagawa Wazanzibar kisiasa na kushindwa kumuenzi marehemu Aboud Jumbe, ambaye pamoja na kuiongoza Zanzibar kwa amani na utulivu pia ndiye aliyemlea Maalim Seif kisiasa.

Alisema tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa marudio uliosusiwa na CUF, Maalim Seif amekuwa akileta chokochoko na uchochezi dhidi ya serikali ya Zanzibar akidai kwamba haitambui na kuwataka wananchi wa Zanzibar kugoma na kuwataka wasilipe kodi kwa serikali.

CHANZO: HABARI LEO

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents