Burudani

TLC watembeza bakuli kukusanya fedha kurekodi album ya mwisho, zaidi ya $200,000 zachangwa

Ikiwa ni siku sita tu tangu waanzishe kampeni yao waliyoipa jina, Kickstarter, kundi la TLC limekusanya zaidi ya dola $200,000.

tlc-nyc

T-Boz na Chilli walianzisha kampeni hiyo ili kuchangisha $150,000 kwaajili ya kurekodi album yao ya tano na ya mwisho.

Hadi Ijumaa, walikuwa wamekusanya zaidi ya $205,000 na bado wana siku 26 za kuendelea kukusanya michango. Mastaa kadhaa nao wamejitokeza kuwachangia wakiwemo Soulja Boy, Russell Simmons na Bette Midler.

Kundi la New Kids on the Block limetoa $20,000 na Katy Perry ambaye ni shabiki mkubwa wa kundi hilo ametoa $5,000.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents