Michezo

Timu zitakazoshiriki kombe la Dunia zaongezeka kutoka 32 hadi 48

By  | 

Shirikisho la Soka Duniani FIFA hatimaye limepitisha mabadiliko ambapo kuanzia mwaka 2016 timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia zitaongezeka kutoka 32 hadi kufikia 48.

Mpango huo ulipitishwa katika mkutano mkuu nchini Uswizi kwa kupigia kura mpango wa kupanua Kombe la Dunia liwe linashirikisha mataifa 48 huku mabara ya Afrika na Asia yakitarajia kunufaika zaidi.

Baada ya mabadiliko hayo, kuanzia katika mashindano ya mwaka 2026, kutakuwa na makundi matatu yenye timu 16 kila moja.

Mpango huo ambao umekuwa ukipigiwa debe na Rais wa shirikisho hilo Gianni Infantino.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments