Michezo

Timu ya Golf Taifa yakabidhiwa Bendera

 

Kikosi cha Taifa cha mchezo wa Gofu cha wanaume kinatarajiwa kukabidhiwa bendera kwaajili ya kushiriki mashindano ya Dunia yatakayo fanyika Nchini Aregentina kuanzia kesho kutwa.


Akizungumza jijini Dar jana kocha mkuu wa timu hiyo,Rodrick John alisema anaamini watafanya vizuri katika mashindano hayo.

Maandalizi tuliyoyafanya ninaamini yatatufikisha mbali kwenye michuano hii ya Dunia yatakayotukutanisha nchi zaidi ya 54 alisema.

Alisema wachezaji wote watakaowakilisha Tanzania katika mashindano hayo kwa sasa wako katika hali nzuri.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kuepeleka timu za wanaume na wanawake katika mashindano ya hayo.

Timu ya taifa ya wanawake inawakilishwa na Hawa Nyeche na Madina Iddy  ambao waliondoka nchini Oktoba 1.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents