Burudani

Timmy Tdat wa Kenya ataja maana ya wimbo wake mpya ‘Trikide’

Msanii wa Kenya, Timmy Tdat ambaye yupo chini ya lebo kubwa nchi humo ya Kaka Empire amefunguka maana ya jina la wimbo wake mpya ‘Trikide’.

Timmy ameiambia Bongo5, wimbo huo unahusu mtu mwenye mapenzi ya kweli kwa mpenzi wake lakini kuna watu wanatokea na wanajaribu kuvunja mapenzi yao.

“Wimbo huo unahusu mtu ambaye ana hofu ya kupoteza mpenzi wake na hufanya kila kitu katika maisha yake ili kuweza kuwa naye. Hata hivyo watu wake wa karibu wanajaribu kuvunja mahusiano yao,” amesema Timmy.

Trikide ni wimbo ambao umetayarishwa na Bizzy B huku video yake ikiongozwa na Enos Olik. Tazama video ya wimbo huo hapa chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents