Habari

Times FM na makampuni rafiki wasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu

Kituo cha redio cha Times FM kwa kushirikiana na makampuni ya MeTL, Shamo, Simba Trailer, Hugo Domingo, M2 Advertising, Ifatar, kampuni ya vipodozi ya Darling walijitolea na kupata chakula cha jioni kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu/hatarishi wanaosomeshwa katika shule ya msingi Wamato kwa udhamini wa taasisi ya Help2Kids.

Mkurugenzi wa Times Fm, akiwasikiliza watoto baada ya kuwahudumia
Mkurugenzi wa Times FM, akiwasikiliza watoto baada ya kuwahudumia

Tukio hilo lililofanyika wiki iliyopita liliambatana na michezo mbalimbali na hotuba zilizolenga katika mipango ya kuisaidia zaidi shule hiyo ya msingi ya Wamato iliyoko eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam ili kuhakikisha watoto hao wanapata elimu bora zaidi kwa maisha ya baadae.

Akiongea na Times FM, mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Basila Chuwa ameishukuru taasisi ya Help2Kids kwa kuendelea kuisaidia shule hiyo kwa kila hali pamoja na makampuni yote yaliyojitokeza kuhakikisha yanakuwa karibu na kituo hicho kwa lengo la kusaidia huku akitoa wito kwa makampuni mengi zaidi kuiga mfano huo kwa kuwa serikali imelemewa.

“Nilikuwa na shirika la wa Canada lilikuwa linaitwa Canadian Christian Child Fund, ile ilinisaidia kwa miaka zaidi ya kumi. Walikuwa wanafanya vitu vingi sana. Walijenga hata majengo haya, walikuwa wanasaidia nguo, walikuwa wanawaangalia hata nyumbani wazazi. Hata sabuni ya kufulia walikuwa wanawapatia na chakula. Lakini sasa hivi…serikali haiwezi kutusaidia kila kitu (serikali yenyewe imelemewa).”

Mwanzilishi wa Shule ya WAMATO, Bi. Basila Chuwa akizungumza
Mwanzilishi wa Shule ya WAMATO, Bi. Basila Chuwa akizungumza

Ameeleza kuwa nia yake ni kuanzia ‘daycare’ sehemu ambayo watoto watakuwa wanaachwa kwa siku nzima wakisoma na kuangaliwa huku wazazi wao wakiwa katika mihangaiko kisha wanawapitia jioni wakielekea majumnbani. Lakini upungufu wa majengo ni moja kati ya kikwazo kikubwa.

Amesema mpango huo wa ‘daycare’ ni bora zaidi ya kuwa na kituo cha kuwatunza moja kwa moja watoto kwa kuwa kufanya hivyo kutaendelea kuwaweka karibu na malezi ya familia na malezi ya kituo pia. Naye Mkurugenzi wa Times FM, Rehure Nyaulawa amesema Times Fm inaendelea kutoa misaada katika jamii na inakuwa sio tu sehemu ya jamii bali sehemu ya msaada pia kadri inavyowezekana na kwamba kwa kipindi hiki wameamua kusaidia pia katika upande wa elimu kwa watoto ili kutengeneza viongozi bora wa baadae.

Watoto

“Times Fm ni radio ambayo inapenda kujishughulisha na shughuli za kijamii katika kusaidia jamii na kama tunavyosema kwamba tusisubiri wafadhili, serikali ama taasisi ije kutusaidia. Kwa sisi wenyewe tunaona kile kidogo tulichonacho tunajaribu kukaa na wadau tunatengeneza mipango tunakuja tunafanya vitu kama hivi vya kusaidia watoto au communities mbalimbali,” amesema Rehule Nyaulawa.

Amesema shirika la M2 Advertising liliguswa na shughuli za awali za kijamii zilizokuwa zikifanywa na Times Fm awali kama kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), kupaka rangi na kutoa vifaa kwa kituo cha polisi cha Kawe, hivyo shirika hilo kaamua kuungana na mazoezi hayo ya kimaendelea na kuyavuta makampuni mengine pia.
Bwana Rehure ameyashukuru makampunii yote yaliyoshirikiana na Times FM na kuendelea kutoa wito kwa makampuni mengi zaidi kuungana na kituo hicho cha radio.

“Hili tulilifanya kama lilivyo na nafikiri ni njia nzuri ya kuanzia au kuwafuata na kuwaambia ‘jamani tulifanya moja basi twendeni kwenye lingine na lingine’, na pia mashirika mengine ambayo yanahisi kwamba yanaweza kufanya basi nayakaribisha.”

Kupitia mtandao wa Twitter, shirika la Help2Kids lilitoa shukurani zake kwa makampuni yote yaliyosaidia katika kukamilisha tukio hilo, “help2kids would like 2 say thank u 2 @M2Advertising & @TimesFMTZ 4 such a wonderful event yesterday. U truly warmed a lot of child’s hearts” Walitweet Help2Kids.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents