Burudani

Timbulo: Kama ‘Usisahau’ usingefanya vizuri ningerudi darasani au shamba

By  | 

Timbulo amefunguka kuwa kama wimbo wake mpya ‘Usisahau’ aliomshirikisha Barakah The Prince usingefanya vizuri ingekuwa sababu ya yeye kuachana na muziki.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One kuwa, waliwekeza zaidi kwenye wimbo huo na ulikuwa ukitegemewa na menejimenti yake pamoja na yeye kufanya vizuri kabla haujatoka.

“Kwa jinsi nilivyokuwa nimeinvest kwenye hii ngoma na jinsi tulivyokuwa tunaitegemea na menejimenti pengine tungekuwa tunaongelea vitu vingine, kama ngoma isingefanya poa. Kwa kuwa investment yake ilikuwa kubwa sana pengine ingekuwa sababu ya mimi kutokuwepo tena kwenye muziki ambao naendelea kuifanya,” amesema Timbulo.

Timbulo ameongeza kuwa kuna uwezekano mkubwa angerudi darasani au hata shamba kulima kama wimbo huo usingeendana na matarajio yake.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments