Burudani

Timbulo awatetea wanaotegemea kiki kwenye muziki

Timbulo amewatetea wasanii wanaotegemea kiki ili muziki wao ufanye vizuri.

Hitmaker huyo wa ‘Usisahau’ amemuambia mtangazaji wa kipindi chas Flavour Express cha Maisha FM ya Dodoma, Silver Touchez, msanii anatakiwa afanye chochote ili muziki wake ufanye vizuri na apate hela ya kujikimu.

“Mimi namsupport mtu yoyote ambaye anajua muziki wake unataka nini. Kwa mfano mtu ameona muziki wake asipofanya kiki hauwezi kuhit basi afanye, kitu kikubwa watu wanatakiwa waelewe hii siyo shule tunatakiwa tufanye mtihani ila mwisho wa siku tunatakiwa tufanikiwe. Kwahiyo fanya vyovyote ili ufanikiwe kama kwa kumuimba mtu, fanya skendo, fanya janja janja, uwe muongo mwisho wa siku ufanye kitu watu wakipende ili upate hela siyo tupo darasani tuangalie nani anaimba sana au nani anajua sana ,” amesema Timulo.

Muimbaji huyo ameongeza kuwa kama unaweza kwenda kwa mganga au kumuomba Mungu wako muombe, fanya ilimradi mwisho wa siku mkono uende kinywani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents