Burudani
Timbaland kufanya collabo na msanii wa Afrika Kusini
Producer na rapper Timbaland atadondoka nchini Afrika Kusini na kufanya collabo na msanii mmoja wa huko kama sehemu ya show Castle Lite. Producer huyo pamoja na rapper Nas wataenda Afrika Kusini mwezi June mwaka huu.
Timbaland atamchagua msanii mmoja wa Afrika Kusini atakayeshirikiana naye. Nas atapanda jukwaani na kusindikizwa na Mi Casa, Spoek Mathambo, Black Coffee, Zakes Bantwini, DJ Clock with Beatenberg, na Reason.