Burudani

Tidal ya Jay Z yasaini dili la $200m

Licha ya kuwa na changamoto nyingi kwa sasa kwenye kampuni ya mtandao wa Tidal, lakini rapper Jay Z ameonyesha ukomavu wake kwenye biashara kwa kufanikisha kuingia kwenye ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya Sprint.

Kwa mujibu wa Billboard, kampuni ya Sprint imetoa kiasi cha dola milioni 200 na kuifanya kampuni hiyo kumiliki asilimia 33 ya Tidal huku zilizobaki zikiendelea kumilikiwa na Jay Z pamoja na wasanii wenzake wengine akiwemo Beyoncé, Kanye West, Alicia Keys, Nicki Minaj na wengine.

“Sprint shares our view of revolutionizing the creative industry to allow artists to connect directly with their fans and reach their fullest, shared potential,” amesema Jay Z baada ya kusaini dili.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Sprint, Marcelo Claure amesema kwa kushirikiana kwa pamoja kutokana na uzoefu waliokuwa nao katika burudani watahakikisha kampuni yao itawavuta wateja wapatao milioni 45.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents