Burudani

TID anadhani Billnass ana tamaa na hayupo real (Audio)

Mnyama TID anadhani Billnass ni mtu mwenye tamaa na hayupo real.

Billnass

Hitmaker huyo wa ‘Chafu Pozi’ alijiondoa kwenye label ya TID, Radar Entertainment na mnyama hajapenda. Akiongea kwenye kipindi cha Funiko Base cha Radio 5, TID alisema pamoja na kuwa ameondoka na amemuudhi, hawezi kumsumbua kichwa tena.

“Kama yeye amekuwa undisciplined, basi namimi nitakuwa undisciplined. Tumemkata kabisa kwenye program zetu, rasmi,” alisema TID.

Awali Billnass alikaririwa akisema kuwa mkataba wake na Radar uliisha kitu ambacho TID amekikanusha.

“Mimi sikuwa na mkataba na Billnass,” alisisitiza. “Mkataba wangu ulikuwa ni maneno tu kwamba namsaidia na yeye alikuwa na nia sana kwamba anataka kusaidiwa, nimemsaidia kwenye wimbo wa kwanza, nimelipia gharama zangu kwenye video pia, hadi hoteli chakula chake, kila kitu mimi nimefanya lakini kitendo cha kutoka bila kuniambia mimi halafu baadaye ananipigia simu kwamba ‘mzee hii ni stunt tu nimetengeneza kwamba mimi nimeondokana na Radar lakini hiyo sio kweli baadaye nitakanusha.’ Kweli hivyo vitu na akili yako unaweza kufanya kwa mtu ambaye anakusaidia? Mimi kwakweli Billnass amenikasirisha sana na sitaki aniharibie kwasababu anaonekanA ni mtu mwenye tamaa tu ya kutaka vitu Fulani,” alisema TID.

Rapper huyo sasa ana kampuni yake iitwayo LFLG inayomsimamia Nuh Mziwanda pia.

Alipoulizwa wiki iliyopita kuhusiana na tofauti yake na TID, Billnass alisema: “Mimi natambua mchango wake na nimewahi kuzungumza mara nyingi na najua nafasi yake kwangu na sijawahi kumdharau na kuondoka Radar halitakiwi liwe kosa.”

Msikilize TID hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents