Burudani

TID afanya kolabo na rapper wa Afrika Kusini, Tumi Molekane

TID ameingia kwenye studio ya B Records za Dar es Salaam na rapper wa Afrika Kusini, Tumi Molekane. Wimbo waliorekodi unaitwa ‘Bongo’.

1742684_293937064132353_272031686_n

TID ameiambia Bongo5 kuwa rapper huyo alikuwa na shauku kubwa ya kufanya naye kazi.

“Mimi na Tumi tumefanya kazi moja nzuri sana studio jana,” amesema TID. “Tumetoka late sana kama saa kumi hivi. Tumerekodi wimbo mpya ambao unaitwa Bongo. Tulikuwa tunawasiliana muda mrefu kupitia social network, tukapata nafasi baada ya kuingia Dar es salaam ndo tukaamua kufanya kazi. Project iko mwishoni kumalizika leo nafikiri tunamalizia kurekodi hajarudi zake South Africa kesho. Mimi nafikiri video yake tunatakiwa tufanyie South Africa muda si mrefu. Jamaa yupo serious kabisa na hii kazi.”

Naye Tumi ameandika; In studio with the very shirtless T.I.D hehe. For real, this dude is crazy talented.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents