Burudani

The Weeknd aingia kwenye orodha ya dhahabu Vevo

Video ya wimbo wa ‘The Hills’ ya The Weeknd imefanikiwa kuingia kwenye orodha ya mtandao wa Vevo ambao unafanya kazi kwa ukaribu na Youtube na kuwa kati ya video zilizowahi kutazamwa zaidi kwenye mtandao huo.

‘The Hills’ ambayo imetoka mwezi Mei mwaka juzi imefanikiwa kufikisha view bilioni moja na kumfanya muimbaji huyo kushika nafasi ya 36 katika orodha ya wasanii ambao wapo katika mtandao huo ambao video za zimetazamwa zaidi wakiongozwa na Justin Bieber kupitia wimbo wake wa ‘Sorry’ ambao umetazamwa zaidi ya mara bilioni mbili.

Kupitia mtandao wa Instagram wa Vevo umempongeza The Weeknd kwa kuandika, “Congratulations to @TheWeeknd! His video for “The Hills” has over 1 BILLION views. Let’s go for 2! Watch it again at the link in our bio. #TheWeeknd#TheHills #1Billion.”

Muimbaji huyo ambaye ana asili ya nchini Ethiopia amefanikiwa kujitengenezea heshima kupitia muziki wake kutokana na kufanya vizuri kwenye chati kubwa mbalimbali duniani ikiwemo ya Billboard.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents