Habari

The Return Of The Ninja: Roma atangaza kuachana na utaratibu wa kutoa single moja kwa mwaka, kuachia single mpya ‘KKK’ wiki hii

Rapper ambaye ilikuwa ni adimu kusikia ametambulisha single zaidi ya mmoja ndani ya mwaka mmoja, Roma Mkatoliki ametangaza ujio wa utaratibu mpya alioamua kujiwekea wa kuanza kutoa single zaidi ya moja kwa mwaka mzima.

ROMA TUZO

Rapper huyo kutoka Tanga ambaye single yake ya mwisho ‘2030’ aliitoa mwishoni mwa mwaka 2012, amesema kuanzia mwaka huu 2014 anaanza utaratibu mpya wa kutoa single tatu kwa mwaka, uamuzi uliotokana na matakwa ya mashabiki wake na pia kutaka kudhihirisha kuwa naye anaweza kutoa nyimbo nyingi kwa mwaka kama wafanyavyo wasanii wengine.

“Kwa takribani miaka sita ama saba nilikuwa na system hiyo ya kutoa wimbo mmoja kwa mwaka toka 2007 tunaanza na wimbo wa kwanza. Lakini time inaenda na vitu vingi vinaenda vinabadilika. Kwa hiyo kitu ambacho Roma anakuja nacho 2014 hatatoa wimbo mmoja kama ilivyozoeleka, nina plan ya kutoa nyimbo kama tatu kwa sababu nyimbo zinarekodiwa kila siku. Kwa hiyo wimbo wa kwanza tunautoa mwanzo wa mwaka, katikati ya mwaka kwenye June hivi naweza kutoa wimbo mwingine na mwishoni mwa mwaka naweza kutoa wimbo mwingine.” Alisema Roma kupitia kipindi cha ‘The Jump Off’ cha Times FM.

Mradi huo mpya wa Roma alioupa jina la ‘The Return of The Ninja’ unaaza wiki hii ambapo anatarajia kuachia wimbo mpya alioupa jina la ‘KKK’, uliofanywa na producer J-Ryder wa Tongwe Records.

“Tunaplan kuitoa siku yoyote kuanzia wiki ijayo yaani kuanzia jumatatu. Inaweza kuwa Jumatatu hiyo hiyo ama jumanne, ama jumatano…unaitwa ‘KKK’ yaani triple K, umefanyika Tongwe records kwa producer J-Ryder pamoja usimamizi mzima wa C.E.O wetu wa Tongwe ambaye ni J-Marder.” Alisema Roma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents