Burudani

The Forbes Five: Wasanii 5 wa Hip Hop wenye mkwanja zaidi – 2013

Hakuna ubishi kuwa Diddy sio rapper mwenye uwezo wa kushtua lakini anajua kutengeneza mshiko. Ni mjasiriamali wa muziki na ndio maana mwaka huu ameongoza list ya jarida la Forbes la wana Hip Hop wenye mkwanja mrefu zaidi.

9854_1

Kwa mujibu wa ‘Forbes Five’ orodha ya wasanii wa hip hop wenye mkwanja zaidi, Diddy ambaye ni mwanzilishi wa Bad Boy Records ana utajiri ufikao dola milioni 580. Utajiri wake unatokana na nini? Fedha nyingi inatokana na biashara yake nje ya muziki kama deal la kilevi maarufu cha Ciroc na biashara zingine kibao.

Namba mbili imeenda kwa Shawn “Jay-Z” Carter, ambaye ameachwa mbaaaaaaaali na Diddy akiwa na utajiri ufikao dola milioni 475.

Jay-Z_11132009_4382-8791

Hov anaendelea kuingiza mkwanja toka deal la milioni 204 la mauzo ya Rocawear mwaka 2007 na mkataba wake wa dola milioni 150 na Live Nation mwaka uliofuatia. Bado ana hisa kwenye label ya Roc Nation pamoja na timu ya kikapu ya Brooklyn Nets na uwanja wa Barclays Center pia. Michongo mingine inayompa mkwanja ni pamoja na ushirikiano na Duracell, Budweiser na D’ussé Cognac.

Nafasi ya tatu imechukuliwa na mchawi wa beats, Andre “Dr. Dre” Young akiwa na utajiri wa dola milioni 350. Yeye ashukuru sana mafanikio ya headphones zake za Beats by Dr. Dre.

drdre_1999_b3_12

Mkataba wake na kampuni ya simu ya HTC uliompa dola milioni 300 August 2011, umeendelea kuwa mnono baada ya Beat by Dre kushikilia asilimia 65 la soko la headphones duniani.

Bitoz wa nguvu Bryan “Birdman” Williams amekamata nafasi ya 4. Akiwa mkuu wa himaya ya Cash Money/Young Money jamaa ana utajiri ufikao dola milioni 150.

leestarnesphoto.birdman-1

Nafasi ya mwisho inakamatwa na Curtis “50 Cent” Jackson mwenye dola milioni 125.

-50Cent-50-cent-6446615-1280-1024

Huyu ni master mwingine wa kutengeneza brand na zikafanya vizuri. Pesa nyingi aliyonayo inatokana na mauzo ya muziki wake, michongo mbalimbali video games na vitabu. Pia hisa alizonazo kwenye brand kama VitaminWater na mauzo ya headphones zake, SMS Audio.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents