Michezo

Thamani ya Cristiano Ronaldo ni Euro bilioni 1 – Wakala

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ni mwanamichezo bora kuwahi kutokea na ana thamani ya euro bilioni 1, kwa mujibu wa wakala wake, Jorge Mendes.

Ronaldo_3_blog

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli 19 kwenye michezo yote 11 katika mashindano yote msimu huu na kuna uwezekano mkubwa wa kushinda tuzo ya Ballon d’Or tena. Mendes – anayedai kuwa Ronaldo ataondoka Madrid akiwa na miaka 40, licha ya tetesi kupewa ofa na Manchester United, anaamini kuwa mteja wake ni mwanamichezo bora zaidi kuwahi kutokea duniani.

“Ni mchezaji bora kwenye mchezo mkubwa duniani wenye ushindani kuliko mingine. Kwa sababu hiyo, ni mwanamichezo bora duniani,” alisema.

Alipoulizwa ni gharama gani ambayo club inayomtaka inatakiwa, Mendes alijibu; “The price that is stated in his release clause – €1bn.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents