Burudani

Thabit Abdul adai muziki wa taarab umeyumba baada ya Mzee Yusuph kuacha kuimbaa

Mpiga kinanda na muimbaji maarufu wa taarabu nchini, Thabit Abdul ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Dunia Imenitupa’ amefunguka kwa kudai kuwa kitendo cha Mzee Yusuph kuacha muziki wa taarab kimeufanya muziki huyo kukosa ushindani.

Akiongea wiki hii katika kipindi cha Joto La Asubuhi cha EFM, Thabit Abdul amedai wakati yupo Mzee Yusuph kwenye game kuna namna fulani muziki wa muzuki wa taarab ulikuwa unachangamka.

“Toka Mzee Yusuph amecha muziki Taarab imeyumba,” alisema Thabit “Na bendi nyingi zimeanzishwa kama watu wamefunguliwa sasa, ushindani hakuna kwa kuwa waimbaji wengi wamezoea kutungiwa,”

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anaimiliki bendi ya taarab ya Wakali Wao, amedai alifanya muziki wa aina nyingi sana ila alishawishika na Taarab ndio maana mpaka sasa yuko kwenye muziki huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents