Burudani

Tetesi: Dida amtambulisha ‘mchumba’ mpya baada ya ndoa yake na Ezden kuvunjika

Kwa mujibu wa gazeti la udaku la Risasi katika ukurasa wake wa mbele, mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko Ya Pwani cha Times Fm, Dida Shaibu amemtambulisha ‘mchumba’ wake mpya katika siku yake ya kuzaliwa alhamisi iliyopita baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake wa ndoa ya tatu, Ezden Jumanne miezi kadhaa iliyopita.

Risasi Dida

Hivi ndivyo ilivyoandikwa na gazeti hilo:

“SIKU chache baada ya kudai hawezi kuolewa kwa sasa, mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’, ameonesha matumaini mapya ya kuolewa baada ya kumwanika mchumba’ke mpya.

Dalili za matumaini hayo mapya zilionekana usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita katika sherehe yake ya kuzaliwa (bethidei) iliyofanyaka nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao Bongo.

dida na shemeji yake
Mtangazaji wa Kipindi wa Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ akimlisha keki Shemeji yake, Feisal.

Wakati sherehe ikiendelea, Dida aliibua minong’ono ya aina yake baada ya kutambulisha uwepo wa shemeji zake waliotoka Arusha ambao walimwakilisha mchumba wake katika pati hiyo.

“Jamani humu ndani kuna watu mbalimbali ambao wamefika kuniunga mkono, mkiwemo wasanii wanahabari pamoja na watangazaji wenzangu, lakini kikubwa zaidi napenda kutambua uwepo wa shemeji zangu waliofunga safari kutoka Arusha, wamekuja kuniunga mkono, nimefurahi sana,” alisikika Dida.

Ulipofika muda wa kutoa zawadi, mmoja wa mashemeji zake hao aliyejitambulisha kwa jina la Feisal alishika kipaza sauti na kusema alitinga kwenye hafla hiyo kumwakilisha ndugu yake (jina alilihifadhi) ambaye alimtuma amwambie Dida kuwa amemzawadia gari lenye thamani ya Sh. milioni 26 za madafu ambalo siku si nyingi litatua Dar.

“Hehee my new baby, huyo ndiye my new baby jamani na hawa ndiyo mashemeji zangu wa ukweli,” alipaza sauti Dida.

Alipoulizwa na mwandishi wetu juu ya mipango yake na mchumba huyo mpya, Dida alifunguka:

“Huyo ndiye mwanaume wangu wa sasa muda ukiwadia nitaanika kila kitu, bado mapema mno kuzungumza mengi,” alisema Dida ambaye kama ataolewa na mwanaume huyo itakuwa ndoa ya nne.

Dida aliyemwagana na Ezden Jumanne miezi kadhaa iliyopita, kabla ya hapo aliwahi kuolewa na wanaume wawili tofauti ambao alimwagana nao kwa talaka.”

Source: Global Publishers

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents