Burudani

Temba kusherehekea siku ya kuzaliwa leo kwa kufanya show itayokusanya pesa kusaidia watoto

Msanii wa muziki Mh Temba leo anatarajia kufanya show ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, itakayofanyika kwenye ukumbi wa Ikweta Grill Temeke, ambapo mapato yatakayopatikana yatapelekwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Temeke.

10354416_620722098037525_1019059746_n

Akizungumza na Bongo5 leo, Fella amesema Temba atasindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo waimbaji wa taarab.

“Maandalizi yapo tayari burudani itakuwa kubwa kwa sababu licha ya kuwepo kwa Wanaume Family, Dogo Janja, Isha Mashauzi pamoja na Yamoto Band wote watakuwepo kuhakikisha burudani inaenda vizuri. Kwakuwa hii ni burudani kwajili ya Mh Temba kusherekea siku yake ya kuzaliwa baadhi ya mapato yatakayopatikana yatapelekwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Temeke, kwa hiyo tunaomba wadau watuunge mkono kwenye hili,” alisema Fella.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents