Technology
Teknolojia: China kutengeneza ‘lifti’ yenye kasi zaidi duniani inayoweza kupanda ghorofa 95 kwa sekunde 45
Kampuni ya Hitachi imetangaza mpango wake wa kutengeneza lifti yenye kasi zaidi duniani (The world’s fastest ultra-high-speed elevator) katika jengo refu la Guangzhou CTF Finance Centre linalojengwa huko Guangzhou, China.
Mchoro wa jengo hilo refu la Guangzhou CTF
Jengo hilo linalotazamiwa kukamilika ifikapo mwaka 2016, litakuwa na lift hizo zenye uwezo wa kwenda kasi ya kupanda au kushuka ghorofa 95 kwa sekunde 45.
Hitachi wamesema lifti hizo zitatumia teknolojia ambayo inahakikisha usalama kwa watumiaji, hivyo wasafiri watakuwa wakisafiri salama na kwa raha pamoja na mwendo wake mkali.
Ujenzi wa kikwangua anga hicho cha CTF ulianza mwaka 2010 na picha hii ilipigwa 23 December 2012, na linatarajiwa kukamilika mwaka 2016.
Source: Daily Mail