Habari

Tecno L9+ kuja kuwa mkombozi wa Watanzania

Kampuni ya simu yenye asili ya China, Tecno Mobile imekuja na ufumbuzi wa tatzo la simu janja (smart phone) kutokaa na chaji kwa muda mrefu.

Tecno wanajulikana kwa kuwa na simu zinazokaa na chaji kwa muda mrefu lakini zikiwa na ubora mkubwa, inatazamiwa hivi karibuni Tecno wataingiza sokoni simu itakayokuwa mkombozi wa watanzania. Simu hii inatoka kwenye mfululizo wa matoleo ya L, ikitanguliwa na L8/l8 plus hii inakuja ni L9 plus.

Tecno L9 plus inatarajiwa na kuwa na betri yenye uwezo mkubwa zaidi simu zilizoko sokoni za aina yake, ikiwa ni 5000 mAh, kwa ukubwa wa betri hii pamoja na matumizi makubwa kusikiliza au kuangalia video, kupiga picha na kutumia mitandao ya kijamii simu hii inaweza kufika masaa 72 ambayo ni sawa siku tatu ndipo mtumiaji anaweza kuchaji tena.

Pia Tecno L9 plus pamoja na kuwa na betri kubwa inakuja ikiwa na uwezo mkubwa kuchaji haraka, mtumiaji akichaji kwa muda wa dakika tano anaweza kuitumia simu kwa kupiga picha zaidi ya 1000.

Kwa watanzania walioko mikoani simu hii inawafaa zaidi hasa ukizingatia matatizo ya umeme kukatika katika kwa muda usiojulikana, pia kupunguza kadhia ya kutembea na vibeba umeme (power bank).

Tecno L9 plus inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni pia ina usalama wa alama ya vidole maarufu kama finger print hali kadhalika wembamba mzuri utakaompa mtumiaji urahisi wa kuitumia.

Inatabiriwa kufanya vizuri sokoni na wataalamu wa vifaa vya mawasiliano, Tecno L9 plus inasubiriwa kwa hamu na watanzania wengi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents