Burudani

TeamWema wanalipiza kisasi kwa Nay wa Mitego kwa njia itakayokuacha mbavu zikiuma

Team Wema wana hasira na Nay wa Mitego baada ya rapper huyo kumchokoza malkia wao kwenye ngoma yake mpya ‘Shika Adabu Yako.’

12543311_165915390449197_1955172136_n

Kwenye wimbo huo Nay anarap:

Wema Sepetu una mimba kweli, au ndo kiki za msimu?
Miezi tisa sio mingi, isije ikakugharimu
Na siku hazigandi tayari ushakuwa bibi
Na unakoelekea utatafuta kiki hadi kwa Fid

Mistari hiyo hawajaipokea vizuri na sasa Team Wema wako kooni kwa Nay wa Mitego wakilipiza kisasi. Wanazitengeneza picha za rapper huyo na kuzikiweka lipstick na mawig/weaving kumpa muonekano wa mwanamke.

12677289_445286425672382_792633554_n

12628052_1675095419440026_595903842_n

Hata hivyo Nay haoneshi kutishika.

Asanteni wapenda muziki mzuuuriii..!! Haya wale waliopanic twendeeee tililikeniiiiiiii ila adabu mmeshika ndio maana mapovu yanawatokaaaa,” ameandika kwenye post mpya ya Instagram.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents