Habari

TBS kuanza kufichua viwanda visivyo rasmi

Shirika la viwango nchini, TBS limefungua ofisi za kanda katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya ili kudhibiti mianya ya uingizaji wa bidhaa hafifu nchini unaofanywa na wafanyabiashara wasio waaminifu.

TBS

Kaimu mkuu wa TBS, Dr Egid Mubofu, amesema, “ofisi hizo zitafanya kazi karibu na wazalishaji viwandani ili wananchi wapate bidhaa zenye viwango.” Hivyo amewataka viongozi wa mikoa hiyo kufichua viwanda vinavyozalisha bidhaa bila kufuata utaratibu.

“Ofisi hizi zitafanya kazi kwa ukaribu wananchi wapate bidhaa bora,” alisema kwa kuongeza kuwa watendaji katika ofisi hizo watakuwa wanafanya ukaguzi viwandani na kushughulika na maombi ya wazalishaji wapya.

Alisema ofisi ya Mbeya itahudumia mikoa ya kanda ya kaskazini ikiwemo Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Arusha yenyewe na ofisi ya Mwanza itahudumia kanda ya ziwa mikoa ya Mara, Kagera, Manyara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza yenyewe.

Ofisi ya Mbeya itahudumia Nyanda za Juu Kusini ya Iringa, Songwe,Ruvuma, Njombe na Mbeya yenyewe.

“Ilikuwa ni vigumu kwa shirika kugundua uwepo wa viwanda bubu katika maeneo ya mikoani na wilayani kwa urahisi kutokana na umbali lakini sasa kazi itafanyika bila kikwazo,” alisema.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents