Diamond Platnumz

Exclusive: Video za Bum Bum na Mdogo Mdogo zimemgharimu Diamond shilingi milioni 130!

Wakati unafurahia kuangalia video kali mbili za Diamond Platnumz, Bum Bum na Mdogo Mdogo zilizoachiwa kwa pamoja jana, tungependa kukufahamisha kuwa ubora huo unaouona haujaja kwa pesa za nyanya.

Bum Bum na Mdogo Mdogo zimemgharimu Diamond dola 78,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 130 za Tanzania.

“Video ambayo tumefanya Uingereza imetucost dola 38,000 video ambayo tumefanya South Africa ambayo ni mdogo mdogo imetucost elfu 40,000,” amesema Tale. Akizungumza kuhusu kuwapata waigizaji kwenye video ya Mdogo Mdogo, Tale amesema walimlipa Godfather kulingana na kile walichohitaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents