Burudani

Taylor Swift avunja rekodi ya Vevo iliyokuwa ikishikiliwa na Nicki Minaj

Muimbaji Taylor Swift ameweka rekodi mpya kwenye mtandao wa video wa Vevo kupitia video yake mpya ‘Bad Blood’ aliomshirikisha Kendrick Lamar.

Video hiyo imevunja rekodi ya Vevo ya video iliyotazamwa zaidi ndani ya saa 24, kwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 20.1 kwa siku ya kwanza iliyowekwa kwenye mtandao huo. Hadi sasa imetazamwa zaidi ya mara milioni 48 ikiwa ni siku ya nne.

Swift ameivunja rekodi iliyokuwa imeweka na video ya Nicki Minaj ‘Anaconda’ ambayo iliweka rekodi hiyo toka August 2014 ya kutazamwa mara milioni 19.6 kwa siku ya kwanza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents