Burudani

Taylor Swift aelezea fundisho alilopata kutokana na beef yake na Nicki Minaj

Taylor Swift amekiri kuwa kuna kitu amejifunza kutoka kwenye beef yake na Nicki Minaj.

Taylor-Swift

Mwimbaji huyo mwenye miaka 23 alipishana maneno na rapper Nicki Minaj kupitia Twitter miezi kadhaa iliyopita, kutokana na nominations za VMAs japo kuwa walishamaliza tofauti zao.

Taylor-Swift-Nicki-Minaj 2

Taylor amesema kitu kikubwa alichojifunza kutoka kwenye beef hiyo ni kuwa, atakuwa akitumia sms kuwasiliana na watu moja kwa moja pale anapokuwa na jambo kuliko kulumbana katika mitandao ya kijamii. Aliongeza kuwa hali kama hiyo ikijitokeza tena atakuwa anautafuta uongozi wa mhusika na kuomba namba ya msanii huyo na kumtumia ujumbe wa maandishi (sms) .

Akizungumza na jarida la NME Taylor alisema, “I don’t want to talk about it but I send text messages now. If there seems to be some kind of misunderstanding, I go to someone’s management, I get their number and I text them. It’s an important lesson for anyone to learn in 2015.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents