Michezo

Tanzia: mcheza kickboxing wa miaka 14 Scott Marsden afariki dunia

Tasnia ya mchezo wa kickboxing imekubwa na msiba mzito baada ya kijana Scott Marsden mwenye miaka 14 kufariki baada ya kuzirai wakati wa pigano la kuwania taji la kitaifa.

Pambano hilo lilifanyika kwenye mji wa Leeds, Uingereza Jumamosi iliyopita lakini kijana huyo alifariki siku ya Jumatatu wakati alipokuwa hospitalini akipata matibabu. Scott alikuwa mwanachama wa muungano wa Marsden All Styles Kickboxing mjini Sheffiled.

Wakati huo huo Jon Geen ambaye ni Rais wa muungano wa shirikisho la mchezo wa Kickboxing duniani nchini Uingereza (WKA) Jon Green amesema, Scott alikuwa mpiganaji anayeheshimiwa sana na wachezaji maarufu wa mchezo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents