Habari

Tanesco yasema hakuna mgao wa umeme, baadhi ya maeneo ya Dar yawa gizani

Badra Masoud

Wakazi wa baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam wataendelea kuwa gizani baada ya meneja mawasiliano Tanesco Badra Masoud kudai kuwa tatizo lililopelekea kukatwa kwa umeme huo ni kubwa lakini sio mgao.

Akiongea na Power Breakfast ya Clouds FM leo, Bi. Masoud amesema katizo hilo la umeme limetokana na kuharibika kwa transformer maeneo ya Oysterbay.

Hitilafu hiyo imesababisha maeneo ya Kinondoni, Mwananyamala, Morroco, Ada Estate, Oysterbay, Magomeni, Kijitonyama na mengine kukosa umeme kuanzia jana.

“Tumehangaika usiku kucha kuwahamisha wateja kuwapeleka kwenye vituo vingine vya Ubungo, Kijitonyama na kituo cha Kariakoo, alisema Badra.

“Hitilafu hii ni kubwa, ya kiufundi zaidi, kwahiyo tutaendelea kutafuta suluhisho au kulitatua kiufundi na kiutaaam.”

Badra amesema hawezi kuhakikisha lini tatizo hilo linaweza kumalizika kwakuwa tatizo limehusisha transformer kubwa.

“Mambo ya kiufundi huwezi kuyatabiri kwasababu unapofungua mashine ndani hujui kuna tatizo gani, kwahiyo hatuwezi kusema ni saa ngapi wateja watakuwa katika hali ya kawaida.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents