BurudaniVideos

Tammy The Baddest: Baba yangu amewahi kuwa muathirika wa dawa za kulevya (Video)

Rapper Tammy The Baddest amesema moja ya changamoto kubwa zilizorudisha nyuma harakati zake kimuziki ni matatizo ya kifamilia.

Ameiambia Bongo5 kuwa baba yake mzazi amewahi kuwa mwathirikika wa dawa za kulevya.

“My dad alikuwa kwenye drug addiction,” amesema. “Na wazazi wangu mimi wamenipata wakiwa wadogo sana, ukiwaona wazazi wangu unaweza kudhani ni kaka yangu na dada yangu. So kwa baba yangu kuwa kwenye drug addiction yaani mimi ndio kwanza niko shule, mama yangu kupata mtoto mlemavu wa viungo vyote ambavyo hawezi kukaa, kutembea, kuongea kufanya chochote mpaka afanyiwe. Mdogo wangu anayenifuata wa kiume hataki kusikia chochote kuhusu shule zaidi ya mpira mimi kama dada unaweza kuona vitu gani nimepitia,” anasema Tammy.

Tammy anasema kwa sasa Mungu amemsaidia mambo yamenyooka kiasi na mdogo wake, Hassan Kabunda anachezea klabu ya Mwadui FC na Taifa Stars.

Hassan Kabunda, mdogo wake na Tammy (mwenye kofia) ni mchezaji wa Taifa Stars na Mwadui FC

Tammy ameachia video ya wimbo wake mpya Mtoto wa Kike.

https://www.youtube.com/watch?v=IitzZ1YTJAI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents