Habari

Tabia za watu ambao hutakiwi kuingia nao mikataba ya kibiashara

Unapofanya biashara za kawaida au rejareja haina shida watu wengine wanastahili kukopeshwa na wengine hawastahili kukopeshwa kutokana na historia ya kutokulipa madeni. Hata hivyo hiyo ni hali ambayo inajitokeza kwenye biashara ndogo ndogo na hata biashara kubwa.

Successful financial plans

Kutokana na hali hiyo ndio maana kwenye biashara kuna mikataba ya kibiashara – namna ya kufanya biashara na mtu fulani au kampuni fulani na kwa mfumo fulani inategemea aina ya mteja au biashara inayotakiwa kufanyika.

Vile vile kuna watu ambao unatakiwa kuingia nao kibiashara katika kufanya biashara pamoja au kufanya miradi fulani pamoja, lazima uangalie vigezo husika kama vitamwezesha mtu huyu kufanya kazi pamoja na wewe. Mambo yafuatayo ni ya msingi na vile vile yanaweza kukusaidia kujua je huyu nifanyenaye biashara au niachane naye;

Usiingie mkataba wa kibiashara na Mtu aliyefilisika.
Mtu aliyefilisika ni mtu ambaye madeni yake yanazidi kipato na mali alizonazo, huyo kwa lugha fupi amefilisika. Hana haki kisheria ya kuingia mkataba wowote wa kibiashara kwakuwa amekosa sifa ya msingi.

Usiiingie mkataba na mtu mgonjwa wa akili
Mgonjwa wa akili ni mtu yoyote si lazima awe mwendawazimu bali kama ana tabia ya kubadilika badilika katika mwenendo wa maisha yake kiasi kwamba anahitaji uangalizi wa kitaalamu kuhusu tabia zake na maamuzi anayofanya. Kisaikolojia anakuwa hayuko sawa (Emotional Unstable), moja ya vitu ambavyo anaweza kuhatarisha mahusiano yenu kibiashara ni pale ambapo anakuwa hayuko sawasawa kiakili  halafu akaingia kwenye biashara fulani au makubaliano fulani ni rahisi kufanya maamuzi ambayo yanaweza yasiwe na tija kwenye kampuni na vile vile kusababisha hasara.

Watu wanaobadilika badilika au kukosa msimamo
Kuna watu wengi wanapenda ushirikiano kibiashara bila kujua faida na hasara za kushirikiana na watu wengine hivyo kujikuta wakifanya maamuzi tofauti tofauti kila wakati. Watu wanaobadilika ni wale ambao huwa hawafuatilii kwa ukaribu makubadiliano ya mwisho na nini kiliafikiwa, hivyo huja na mawazo mapya kabisa kana kwamba hakujawahi kufanyika maamuzi ya kitu fulani. Watu wa jinsi hiyo utawajua hata kwenye maisha ya kawaida ni kwamba hata mkikubaliana leo kesho atakuja na maamuzi mengine hivyo kurudisha nyuma kazi zetu.

Msiingie mkataba wa kufanya biashara na mtu ambaye hana mawazo ya kibiashara kichwani kwake
Kuna watu wanaofikiri wakitoa hela basi kila kitu kitaenda hivyo huwaachia watu wengine ndio wawajibike kufanya biashara. Watu wa namna hiyo unatakiwa kuwakwepa kama ukoma, hao ni wanyonyaji. Kama nilivyotangulia kusema kuna watu wanaiga biashara lakini hawana uwezo wa kufanya biashara na hawataki kujifunza biashara ila wanataka kufanya biashara hao epukana nao kwakuwa hawana ujuzi unaohitajika kibiashara.

Unachotakiwa kujua ujuzi wa biashara ni muhimu sana kama ujuzi wako hapo kazini kwa mwajiri wako, hivyo biashara nayo inahitaji watu wenye uwezo wa kibiashara ili biashara ifanyike. Ujuzi huo ni kama, ujuzi kwenye mambo ya fedha, masoko, bidhaa, kuhudumia wateja, utoaji wa huduma n.k

Watu wenye matumizi makubwa, yaani kwao biashara sio kitu cha msingi sana bali wana matumizi makubwa kwenye vitu ambavyo si vya kibiashara hao achana nao

Si watu wote wanajua thamani ya kuwekeza kibiashara na hivyo huingia kufanya biashara kwa kufuata mkumbo. Kwa namna moja ama nyingine utajikuta wanakuja kuomba mfanye biashara pamoja, lakini ishu kubwa ni kwamba wana matumizi makubwa kuliko biashara yenyewe inavyotakiwa kuendelea.

Mfano kama mmeanza biashara fulani na kila mmoja wenu kuna matumizi ambayo anatakiwa kupata kutokana na biashara lakini uwezo wa biashara na matumizi yenu haviendani inapaswa kuweka mpaka wa kuhakikisha kwamba matumizi yenu kwa mwezi ni laki nne kila mtu zaidi ya hapo mtu atatoa hela mfukoni kwake. Ikishindikana kufanya hivyo, faida ya biashara itaathiriwa vibaya.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents