Burudani
T.I. asaini mkataba mnono na Warner Bros Television
Kampuni ya Warner Bros Television imemsainisha mkataba rapper T.I.
Kupitia mkataba huo, studio hizo zitatengeneza series mpya kwaajili ya rapper huyo na pia kumuingiza kwenye miradi mingine inayoendelea.
Kwenye televisheni, T.I. amewahi kuigiza kwenye tamthilia ya House Of Lies ya Showtime na Boss ya Starz.
Hivi karibuni alimaliza kutayarisha msimu wa tano wa reality show yake The Family Hustle kupitia VH1.