Michezo

Swansea kumkosa Nathan Dyer msimu mzima

Mchezaji wa klabu ya Swansea Nathan Dyer atakua nje ya uwanja mpaka mwisho wa msimu wa ligi kuu nchini Uingereza.

Winga ambaye ana umri wa miaka 29, aliumia mshipa wa kifundo cha mguu katika mchezo wa ligi dhidi ya Leicester City siku ya jumapili .

Nyota huyu raia wa Uingereza amecheza michezo mitano toka Paul Clement ateuliwe kuwa meneja wa Swansea mwezi uliopita .

Swansea pia wataendelea kumkosa winga wao mwingine Jefferson Montero anyesumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents