MichezoMitindo

Swahili Fashion week Yazinduliwa Nairobi

Mustafa_Hassanali_briefing_the_Media_on_his_left_is_USAID_Compete_Representative_Finn_Holm-Olsen_and_on_the_right_Redds_Kenya_Marketing_Manager_Pinkie_Nyandoro-33 

Wiki ya ubunifuwa  mitindo ya Kiswahili almaarufu kama” Swahili fashion week 2011” inatarajiwa kuanza rasmi siku ya tarehe 10 mwezi wa kumi na moja mpaka tarehe 12 ya mwezi huu katika viwanja vya ofisi za zamani za bunge Karimjee.

Wiki hiyo ya ubunifu wa mitindo ya Kiswahiliambayo  kwa mwaka huu inaingia mwaka wake wan ne tangu kuanzishwa kwake rasmi mwaka 2008 itajumuisha wana mitindo mbali mbali 50 kutoka ukanda wa nchi zinazoongea Kiswahili ikiwemo kujadili mustakabali wa ubunifu kwa siku za usoni kwa nchi za ukanda zinaz ongea  kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Nairobi nchini Kenya siku ya tarehe 2 ya mwezi huu katika shughuli ya kutambulisha tamasha hilo, muasisi wa tamasha hilo la wiki ya mitindo ya Kiswahili bwana Mustafa Hassanali alisema “Tamasha hili la ubunifu wa mitindo ya Kiswahili limekuwa maradufu hivyo basi kwa sasa tunalitambulisha tamasha hili katika shirikisho la Afrika Mashariki kupitia tasnia ya ubunifu na mitindo, tunachukua pia fursa hii kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara”.

Tayari wabunifu wane kutoka Kenya wamepata mwaliko rasmi wa kushiriki wiki hiyo ya mitindo ya kiwahili ambapo wabunifu hao ni Patricia Lulu Mbela wa Poisa, Rachel Mutindi wa  KI2 Collection, Vera vee Ochia kutoka  Malindi na Sonu Sharma wa nyumba ya mitindo “ just like that”.

Redds_Kenya_Marketing_Manager_Pinkie_Nyandoro_Addressing_the_Media_on_her_right_is_USAID_Compete_Representative_J_C_Mazingue-133

Naye meneja masoko wa kinywaji cha Redds original Pinkie Nyandoro alitoa nasaha zake kwa kuwatakia kheri washiriki hao wane  wateule wa ubunifu kutoka Kenya na kuwataka kuonyesha uwezo wao wa hali ya juu katika wiki hiyo ya ubunifu na mitindo ya Kiswahili jijini dar-es-salaam.

Katika wiki hiyo ya mitindo mwaka huu pamoja na maonyesho ya nguo za mavazi kunatarajiwa kuwemo zaidi ya vibanda 40 ambazo vitafanya biashara mbali mbali za mauzo ya bidhaa za nguo na vifaa mbali mbali vinavyotumika katika kutengeneza mavazi hayo.

Cross_section_of_kenyan_Media_who_attended_the_Swahili_Fashion_Week_media_Briefing_on_Nov_2__hosted_by_Redds_original33333

Aidha katika sherehe ya ufunguzi wa wiki hiyo ya mitindo ya Kiswahili waandaji wanatarajiwa kwa mara ya kwanza kutoa tuzo kwa wabunifu wan chi zilizo ukanda wa afrika Mashariki na kati wakisherehekea mafanikio yaliyopatikana katika tasnia hiyo sio tu kwa wadau wa fani hiyo Tanzania pekee bali ukanda unaozunguka nchi hizo.

Nayo Kampuni ya utoaji wa huduma ya usafirishaji wa anga Precision Air wamesema katika kuunga mkono juhudi za muunganiko wa jumuiya ya Afrika Masharikiwao kama  shirika la ndege linalofanya vizuri katika ukanda wa Afrika Mashariki hawana budi kujitolea kuwa msafirisha rasmi wa Tamasha hilo la mitindo na ubunifu wa Kiswahili kwa mwaka huu kama sehemu ya kuunga mkono tasnia hiyo ya ubunifu na mitindo alisema .

Wakimalizia katika taarifa hiyo kwa waandishi wa habari moja ya wadhamini wa matukio ya kijamii kutoka katika taasisi ya kutoa  misaada ya kijamii ubalozi wa Marekani yaani USAID ambao wamekuwa wakidhamini elimu ya biashara na masoko katika kazi za ubunifu wamesema meneja mkazi wa shirika hilo jijini Nairobi bibie sarah Wachira.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents