Burudani

Sugua Gaga ya Shaa yavusha views milioni 11 kwenye Youtube

Sugua Gaga ya Sarah Kaisi aka Shaa, ndio video ya msanii wa Tanzania iliyowahi kuangaliwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube tangu kuwepo kwake.

SHAA

Video ya wimbo huo sasa ina views zaidi ya milioni 11 kwenye mtandao huo tangu iwekwe takriban miezi saba iliyopita.

Video ya wimbo huo iliongozwa na Adam Juma na inahusisha wanawake wa uswahili wakicheza mtindo maarufu ya uchezaji katika maeneo ya uswazi.

Hivi karibuni Malkia huyo wa Uswazi alionesha furaha yake baada ya video hiyo kufikisha views milioni 10.

“10Million views… Ahsanteni saaaaana emojiemojiemoji #10MillionViews #SuguaGaga,” aliandika Shaa kwenye Instagram. Mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwa msanii huyo wa kundi la zamani la Wakilisha.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents