Burudani

Sugu kuirudisha brand ya Deiwaka kivingine

Rapper mkongwe na mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu amesema brand Deiwaka inarudi kivingine baada ya kufeli kwenye upande wa production.

Sugu

Miaka kadhaa Sugu aliahidi kufungua studio yake ya ‘Deiwaka’ lakini dili hilo lilionekana kufeli baada ya kuibiwa vifaa vyote alivyokuwa amenunuwa kwa ajili ya studio hiyo.

Akiongea kwenye kipindi FNL, kinachoruka kupitia EATV, Sugu alisema ‘Baada ya kufeli kwa studio ya Deiwaka sasa hivi Deiwaka inarudi kwa njia nyingine’.

“Ni kweli nilikuwa na mipango ya kufungua studio, lakini baada ya siku chache vifaa kutua vikaibiwa nilikata tamaa. Lakini brand ya ‘Deiwaka’ bado ipo ila kwa sasa itakuja kivingine japo kwenye upande wa studio ilifeli,” aliongezea.

Kwenye video ya ‘Freedom’ ya Sugu kinaonekana kilevi kiitwacho ‘Deiwaka Gin’ ambacho ni sehemu ya brand hiyo.

33C0756600000578-3569871-image-a-79_1462225848598

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents