Videos

Stoppa Rhymez: Sitegemei tu muziki, mimi ni ‘Professional Electrician’

Rapper wa Arachuga Stoppa Rhymez amesema hakuja Dar es Salaam kufanya muziki peke yake bali kuja kufanya kazi aliyoisomea ya fundi umeme.

“Nimeamua kuja Dar kikazi zaidi siyo music tu, mimi ni professional electrician,” ameiambia Bongo5.

“Kwahiyo kukitokea kuna kazi mbalimbali kufanya wiring kwenye majumba nitakuwa nafanya kwasababu sitegemei music ingawa upo kwenye damu.”

Kuhusu kazi mpya ya kundi lake la Waturutumbi, Stoppa amesema, “Kwa muda mrefu sana watu walikuwa wanahoji Waturutumbi vipi hatusikii ngoma zao kama siku tatu zilizopita tumeingia studio tumerecord ‘Toka mitaa’ wimbo huu umewashilikisha members wa Waturutumbi, watatu mimi niwa nne. Kwahiyo ngoma ya ‘Toka kitaa’ sasa hivi ipo hewani na ni nyimbo ya kwanza official kutoka kwa Waturutumbi, natarajia kufanya video ili niendelee kuuburst.

Kuhusiana na ushiriakiano wa wasanii wa Hip Hop wa Arusha na wa Dar es Salaam amesema, “ni mkubwa sana ni kama ndugu ndiyo maana kwa pamoja tulikuwa tukipiga kelele Arush ,Arusha mpaka watu sasa hivi imefika sehemu wanachukia wanaona wanajidai lakini sisi tulikuwa tunaifagilia home yetu, kitambo sana watu walikuwa wanaona Dar es salaam ndio kila kitu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents