Michezo

Steven Gerrard arudi Liverpool, kuwa kocha wa kikosi cha wachezaji chipukizi

Nahodha wa zamani wa Liverpool na England Steven Gerrard atarejea katika klabu hiyo ya Ligi ya Premia kama kocha wa kikosi cha wachezaji chipukizi.

Gerrard, 36, ambaye alichezea Liverpool mara ya kwanza 1998, ataanza kazi Februari.

Kiungo huyo wa kati aliondoka Anfield mwishoni mwa msimu wa 2014-15 na kujiunga na klabu ya LA Galaxy inayocheza ligi kuu ya soka ya Marekani na Canada (MLS).

Alistaafu uchezaji soka Novemba baada ya kucheza kwa miaka 19.

“Ni kama kukamilisha mduara, kurejea pahala ambapo yote yalianzia,” Gerrard amesema.

“Nilipojua kwamba ningerejea, nilitaka kurejea katika nafasi muhimu. Hii inanipa fursa ya kujifunza na kujiboresha kama mkufunzi, na vile vile kutoa ujuzi wangu, mawazo na tajriba kwa wachezaji hawa chipukizi katika kipindi muhimu sana katika ukuaji wao,” amesema.

Gerrard alihusishwa na kazi ya meneja klabu ya MK Dons baada yake kuondoka LA Galaxy.

Amekuwa akisomea leseni yake ya ukufunzi ya Uefa, ambayo anahitajika kuwa nayo ndipo awe mkufunzi Ligi ya Premia.
Gerrard alichezea Liverpool mechi 710, na kushinda vikombe tisa.

Ndiye mchezaji wa nne kwa kuchezea England mechi nyingi zaidi za kimataifa, mechi 114.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents