Bongo Movie

Steve Nyerere anusurika kuvamiwa na watu wenye mapanga

Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steve Nyerere amesema jana wakati anaelekea nyumbani kwake amenusurika kuvamiwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga.
Mwenekiti wa bongomovie Steve Nyerere

Kupitia Instagram Steve ameandika:

Eeeeeeee Mungu leo nilikuwa na kikao ca PSPF asubuhi jioni ndugu yangu rafiki Devis Mosha akatualika kwake badaye nikawa na wageni wangu toka shinyanga wakati narudi home nilinzingirwa na gari mbili nakulazikisha nishuke bahati nzuri ikapita gari ambayo watu wananijua na kuniokoa Mungu niokoe baba.

Akieleza kwa urefu zaidi, Steve ameiambia Bongo5: Mimi nataka kusema kwamba kila jambo mwenyezi Mungu anaweza kukuepusha atakavyo. Kwahiyo namshukuru Mungu wale walishuka kwenye gari wakiwa na vitu, kwahiyo walivyoshuka kwenye gari wakashuka na vifaa vyao mapanga nini, sasa nyuma yangu kulikuwa kuna watu wenyeji wa Leaders ndio wakaniokoa wakasema ‘Steve usishuke hao watu wana vifaa watakuumiza’ sasa hilo ndio lililoniokoa. Kwahiyo walishuka na nia mbaya sio nzuri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents