Burudani

Stereo na Chid Benz kuachia wimbo ‘Ukonga na Ilala’ mwezi huu

Rapper Stereo anatarajia kuachia kazi yake mpya ‘Ukonga na Ilala’ aliyomshirikisha rapper kutoka Ilala Chid Benz.

page

Akizungumza na Bongo5 leo, amesema kazi hiyo iliyotayarishwa kwenye studio ya Tongwe Records ni wimbo wa kuburudisha pamoja na kuwakilisha sehemu walizotoka.

“Kuna wimbo unaitwa Ukonga na Ilala ambao umeandaliwa na Tongwe Records, Mungu akipenda mwezi huu machi wimbo utaingia mtaani kwa sababu kikubwa sana ninachokisubiria kwa sasa ni kumaliza michakato ya art work, kwahiyo kitu kikubwa kwenye huu wimbo ni kuwakilisha sehemu tunazotokea, kuna watu wetu wengi wapo nyuma ya muziki wetu, pia sisi ni waburudishaji tunafanya kazi ya kuwapa watu burudani, kwahiyo watu wakae mkao wa kula wimbo upo tayari,” alisema Stereo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents