Burudani

Stereo azungumzia matunda ya kubadilisha muziki wake

Rapper Stereo ambaye ameachia wimbo wake mpya uitwao ‘Wako’ aliomshirikisha muimbaji wa Kenya, Victoria Kimani amezungumzia mafanikio aliyoyapata baada kuachia wimbo ‘Usione Hatari’ akiwa na Ben Pol.
StereoBenPol500_full

Akizungumza na Bongo5 leo, Stereo amesema baada ya kuachia wimbo huo, amepokea maoni mazuri huku baadhi ya watu huku wakidhani kuwa ndio wimbo wake wa kwanza.

“Kipindi nafanya hard core rap watu wote walikuwa wanamfahamu Stereo ni nani, lakini kuna upande wa pili ambao ni hawa vijana wa siku hizi, hawa wa kizazi kipya nikaona watakuwa hawapendi kusikiliza muziki ule. Sasa kinachotokea tunaichukua rap ile ile Iakini najaribu kuipeleka katika mitindo mingine ili kuweza kuwafikia na wao,” amesema rapper huyo.

“Nimeona matokeo mazuri kwenye ‘Usione Hatari’, nimepata deal, kwa upande huu tuweze kuendelea kuishi katika muziki huu, kuangalia na watu wa upande wa pili, wale watu ambao wanashabikia aina nyingine ya muziki ili kuweza kuchanganya na kuwapata mashabiki wa muziki wa Hip Hop na muziki mwingine. , Kuna mashabiki ambao nimewapata ambao hawapendi sana Hardcore rap, kwahiyo nimeona nimebadilika kidogo nimeona ninaweza kula vizuri, ninaweza kuvaa na usafiri pia utapatikana,” ameongeza.

“Pia hivi karibuni nilipigiwa simu na kampuni moja ya simu kuna issue za matangazo nikashaanga wananiambia ‘umekuja vizuri’ yaani wananiona mimi ni msanii mpya na huu wimbo niliyofanya na Ben Pol ni wimbo wangu wa kwanza.”

Katika hatua nyingine Stereo amesema anajipanga kukusanya fedha ili mwakani arudi shule kuchukua degree ya pili.

“Muziki unakaa vizuri, sasa hivi nimeanza kuona watu wananipigia simu, wanataka tubargain kuhusu kupatana ,tofauti na mwanzo mtu anataka kufanya show kwa pesa aliyoandaa. Kwahiyo sasa hivi kikubwa ni kufanya muziki ili maisha yaendelee. Mwakani nina mipango ya kwenda kupata degree ya pili kwahiyo pesa zinahitajika.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents