Burudani

Stereo ataja sababu ya kupotea kwa kundi la Sisi

Rapper Stereo amefunguka sababu ya kundi la Sisi lililokuwa linaundwa na Nikki Mbishi, One Incredible na yeye mwenyewe kupotea baada ya muda mfupi tangu kuanzishwa kwake.

Akiongea katika kipindi cha FNL cha EATV, Stereo amedai kuwa fedha na mawazo ya watu wazima ndio chanzo cha kutofanya vizuri kwa kundi hilo.

“Tuongee ukweli, ili tuendelee kuwapa zile ladha ambazo mnakuwa mnazihitaji basi atokee mtu mzima kama alivyokuwa Patrick na Juku waje wasimame. Yaani Mimi, Nikki na One tusifanye chochote ila sisi kazi yetu iwe kuingia studio kurekodi lakini tusikae sisi kama sisi kwa sababu hakuna kitu ambacho kinaweza kufanyika,” amesema Stereo.

“Nikki ni mtu mzima ana mawazo yake, One pia and so am I, kwahiyo tunahitaji labda mtu akae kwamba sikilizeni pesa hizi hapa tufanyeni kazi kitu hiki kinaweza kuendelea,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents