Siasa

Stars Yapokelewa Kishujaa Dar

Maelfu ya mashabiki wa soka wa jijini Dar es Salaam jana walijitokeza katika mitaa mbalimbali ili kuilaki timu ya taifa, Taifa Stars iliyorejea nchini kutoka Sudan baada ya kufanikiwa kukata tiketi ya kushiriki fainali za kwanza za Kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN).

Maelfu ya mashabiki wa soka wa jijini Dar es Salaam jana walijitokeza katika mitaa mbalimbali ili kuilaki timu ya taifa, Taifa Stars iliyorejea nchini kutoka Sudan baada ya kufanikiwa kukata tiketi ya kushiriki fainali za kwanza za Kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN).

Umati ulianza kujikusanya saa mbili asubuhi katika mitaa mbalimbali kuanzia barabara ya Nyerere, ambapo kila walipokuwa wakipita watu walikuwa wakilitaja zaidi jina la kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo na wengine wakiamua kukimbia mchakamchaka na gari hilo.

Timu hiyo, ambayo iliwasili nchini majira ya saa 3: 15 asubuhi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ililakiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye alifuatana na viongozi mbalimbali wa serikali.

Stars iliyoanza msafara wake kutoka katika uwanja huo wa ndege saa 4: 18 asubuhi ilikuwa inashangiliwa na mashabiki hao waliojipanga katika barabara za Nyerere, Uhuru, Msimbazi, Morogoro, Bibi Titi na Azikiwe na hatimaye kuishia katika hoteli ya Kempinski kwa ajili ya kupata chakula cha mchana.

Mashabiki wa soka waliokuwa wanaishangilia timu hiyo walikuwa wakiselebuka muziki uliokuwa unapigwa na bendi ya muziki wa dansi ya Akudo pamo�ja na wachezaji wa Stars na kusababisha mara kadhaa polisi waliokuwepo kuwaamuru wachezaji hao kupanda katika gari la wazi waliloandaliwa na kuendelea na safari.

Waliotia fora zaidi walikuwa Mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji katika kusakata muziki huo na Haruna Moshi `Boban`, huku wakiwa wamevua fulana walizokuwa wamevaa huku mbunge huyo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Operesheni Ushindi akiamua kuvua koti na shati alilokuwa amevaa.

Hali hiyo ya shamrashamra ambayo ilionekana kuzidi katika maeneo ya Karume na Mnazi Mmoja ilisababisha msafara huo kuchukua muda wa saa manne kufika katika hoteli ya Kempinski ambako ndio ilikuwa mwisho wa msafara huo.

Mbali na burudani ya bendi ya Akudo pia kulikuwa na pikipiki maalumu zilizoandaliwa ili kuongeza mbwembwe katika mapokezi hayo.

Waziri Pinda aliwaeleza wachezaji hao kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amefurahishwa na ushindi huo na kuahidi kuandaa utaratibu wa kukutana na wachezaji hao ili kuwapongeza mara atakaporejea kwenye ziara ya kikazi nchini Msumbiji.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents