Burudani

Stamina: Siwezi kuoa msanii, wanazungukwa na vishawishi vingi!

Rapper wa Morogoro, Stamina amezungumzia sifa za mwanamke atayekuja kumuoa na kufanya naye maisha huku akidai kuwa hatathubutu kumuoa mwanamuziki kutokana na mazingira magumu wanayopitia.

Stamina

Stamina ameimba Bongo5 kuwa wanadada wengi kwenye muziki wanaharibiwa kutokana na changamoto wanazopitia mpaka kuhit.

“Sisi tunaishi kwenye muziki hapa pamoja na dada zetu hawa hawa tunaofanya nao tour ndio tuko nao kwenye muziki. Vitu vinavyotokea kwenye muziki na wote wakiwa kwenye tour tunaviona. Mazingira ni kitu kibaya sana, unaweza ukupanga kufanya kitu fulani lakini mazingira yakakufanya.. mimi nisikufiche nataka mwanamke wangu asinijue mimi nani, japo nina mpenzi, mwanamke mwanamuziki simhitaji kabisa. Mimi nakwambia ukweli, hii reality nakupa la ame la kibongo. Huu ni uhalali kwa upande wa wanawake, hii anaijua kila mtu wanawake kwa game ya kibongo wanapitia magumu mengi sana. Wanamke ni rahisi kutoka kwenye muziki lakini pia vikwazo vingi sana mpaka atoboe kutokana na surrounds zilivyo. Kwa wawezeshaji ndio hao hao wana tamaa, studio kuna tamaa, tena kama ndo akiwa mzuri heh kazi anayo! Kwahiyo unaweza ukaona kwamba kuna vitu vingi sana vipo hapo katikati. Kwahiyo mimi binafsi siwezi kuoa mwanamke wanamuziki.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents