Burudani

Stamina: Siwezi kufanya video ya gharama kubwa

Msanii wa Hip Hop, Stamina amedai kuwa kamwe hatofanya video ya gharama kubwa wakati muziki wake bado unamlipa pesa kidogo.

Stamina

Stamina ameiambia Bongo5 kuwa kipato anachopata kwenye muziki hakijamshawishi kufanya video ya gharama kubwa.

“Kwanza siwezi kufanya video ya gharama kubwa hilo sahau,” amesema. “Yaani kusema nifanye video ya milioni 80 wakati nachokiingiza hakipo hivyo. Kwanza sina management, sina promoter. Maisha yangu naendesha mimi kama mimi na muziki wangu, cha msingi ni kufanya video kali, video ya ‘Uko Kwenu Vipi’ inakuja pia kuna video ya wimbo mpya inakuja kwahiyo watu waendelee kusubiri muziki mzuri.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents