Michezo

Spain yapoteza mechi ya kwanza ya kufuzu Euro 2016 baada ya miaka 8

Timu ya taifa ya Hispania jana usiku ikiwa ugenini ikicheza mchezo wao kugombea kufuzu Euro 2016 dhidi ya Slovakia, ilijikuta ikifungwa katika kipindi cha kwanza kwa makosa ya kipa Iker Casillas aliyefanya uzembe wa ajabu na kuruhusu Slovakia kupata goli la kuongoza kupitia free-kick iliyoenda moja kwa moja ndani ya nyavu.

s48

Katika dakika 83, mchezaji wa Spain, Paco Alcacer alisawazisha na mashabiki wengi wakajua mchezo huo utaisha kwa sare lakini goli la mchezaji wa zamani wa Chelsea na Rangers, Miroslav Stoch likaipa Slovakia ushindi katika dakika 87 dhidi ya mabingwa watetezi wa Ulaya.

Baada ya mchezo huo wachambuzi wa soka wamesema sasa inabidi apewe nafasi David De Gea na Iker Casillas apumzishwe. Hii ni mechi ya kwanza kwa Spain kupoteza katika hatua ya kufuzu michuano ya Ulaya au kombe la dunia katika kipindi cha miaka 8. Diego Costa bado hajafanikiwa kuifungia Spain goli tangu alipoamua kuitumikia timu hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents