Burudani

Sony yaamua kuitoa filamu ya ‘The Interview’ licha ya vitisho vya Korea Kaskazini

Sony Pictures imedai inatafuta njia tofauti ya kuitoa filamu yake ya komedi, ‘The Inteview’ baada ya kuahirisha kuizindua kwenye majumba ya sinema siku ya Christmas kutokana na shambulio la mtandaoni lililofanywa na Korea Kaskazini.

the-interview
Waigizaji kwenye filamu hiyo, Seth Rogan na James Franco

Kampuni hiyo imesema ilikuwa inafanya utafiti wa kupata njia mbadala ya kuwawezesha kuizundua filamu hiyo kwa namna nyingine. Rais Barack Obama alisema kampuni hiyo ilifanya makosa kuahirisha uzinduzi wake.

“Hatuwezi kuwa na jamii ambayo dikteta mmoja sehemu fulani anaweza kuanza kuweka ukaguzi Marekani,” alisema. Aliahidi pia kuwa Marekani itajibu shambulio hilo la mtandaoni katika njia watakayochagua.

FBI imedai kuwa Korea Kaskazini imehusika kwenye shambulio hilo japo yenyewe imekanusha. Filamu ya The Interview inaonesha kuuawa kwa kiongozi wake, Kim Jong-un.

Hata hivyo Mwenyekiti Mtendaji wa Sony Pictures, Michael Lynton amemjibu Rais Obama kuwa kampuni yake haijafanya makosa kusitisha uzinduzi wake.

“Naomba tueleweke – uamuzi pekee tuliouchukua kuhusiana na uzinduzi wa filamu hii ni kwenye majumba ya sinema siku ya Christmas baada ya wamiliki kugoma kuionesha,” yalisema maelezo yake.

“Bila majumba ya sinema, tusingeweza kuizindua kwenye Christmas. Hatukuwa na namna. Bado imani yetu ni kuwa mtu yeyote anayetaka kuiona filamu hii atakuwa na fursa ya kufanya hivyo.”

Hackers waliionya Sony kuwa wangefanya tukio la kigaidi kama la tarehe 11 September, 2001 kama filamu hiyo ingeoneshwa kwenye majumba ya sinema.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents